Departments Kiswahili
hod Kiswahili image

Idara ya Kiswahili shuleni mwetu ni idara tunayoienzi sana walimu pamoja na wanafunzi. Tunaienzi kwa kuwa tunakienzi Kiswahili ambacho kina hadhi kubwa nchini kama lugha ya taifa na pia lugha rasmi.

Kwa sasa idara hii ina walimu sita waliohitimu na wengineo wenye taji riba ya miaka mingi. Wana idara hawa ni Bi. Maribe (ambaye pia ni Naibu wa Mwalimu mkuu), Bi. Kagoma, Bw. Karagu, Bi. Mwangi, Bi. Mwanamisi na Bi. Matu.

Walimu katika idara hii wanaushirikiano na mshikamano mkumbwa. Pia wanauhusiano wa karibu na wanafunzi jambo ambalo tunaamini litatusaidia kufikia lengo letu. Tunafanya mengi kuleta ufanisi katika idara na katika matokeo ya mtihani wa 2015 na miaka ya baadaye. Miongoni mwa yale tunayofanya ni kuwashirikisha wanafunzi katika kongamano za Kiswahili na pia kuwashirikisha katika midahalo tosha ya jinsi ya kujibu maswali mbalimbali.

Lengo letu ni kupata alama 9.0 katika mtihani wa 2015. Tuna Imani kuwa tutafikia lengo letu kwani mwalimu mkuu Bi. Teresa Mwangi anatuunga mkono kwa hali na mali. Amehakikisha tuna vitabu vya kutosha na vifaa vingine muhimu tunavyohitaji. Tutaendelea kulenga juu Zaidi mwaka baada ya mwaka.

Mrs. Mwangi P - Mkuu wa Idara ya Kiswahili